Tanzania
ni nchi iliyobarikiwa kuwa na maeneo mengi ya maji kama vile mito, maziwa,
mabwawa na bahari. Maeneo haya ya maji, yamekuwa ni sehemu mojawapo inayotumiwa
na watanzania kwa usafiri pamoja na shughuli zingine za kijamii kama vile uvuvi
na kadhalika.
Pamoja
na utajiri huu ambao tumetunukiwa na Mungu, Tanzania imekuwa ni miongoni mwa
nchi ambazo zinaongoza kwa vifo visivyokuwa vya lazima vitokanavyo na ajali za
majini na majanga mengine ya maji kama vile mafuriko. Hata hivyo historia
inaonesha kuwa katika ajali za majini, watu wengi wanaopoteza maisha huwa ni
wanawake na watoto.
Idadi
hii inakuwa kubwa kutokana na ukweli usiopingika kuwa, wanawake wengi hawana
uelewa wa kitaalamu kuhusu namna ya kujiokoa katika majanga ya maji, hawana
uelewa kuhusu namna ya kukaa katika maji kwa muda mrefu ili kusubiri msaada
panapotokea matatizo ya majini, vilevile hawana uelewa ni namna gani ya kutoa
msaada kwa mtu aliyezama maji. Kutokuelewa kwa mambo haya, kunasababisha
mwanamke awe muoga katika kupambana na majanga ya maji, hivyo kuwa ni muhanga
mkubwa katika majanga yatokananyo na maji.
Hivyo
basi kutokana na tatizo hili lililopo katika jamii yetu ya kitanzania, na kwa
kuwa TANZANIA MARINE SWIMMING CLUB inayo wataalamu wenye uelewa wa majanga ya
maji na ambao wameshahusika katika shughuli za uokoaji katika mafurika ambayo
yalishawahi kutokea maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania, Tanzania Marine
Swimming Club imeamua kuanzisha “program” iitwayo MV MAMA.
MV
mama ni programu inayohusika na utoaji wa elimu kwa nadharia na vitendo kwa
wanawake, kuhusu namna ya kujiokoa na majanga ya maji.
Programu hii ya MV mama, itakuwa na "Event" ambazo zitafanyika katika nyakati tofauti na mikoa tofauti ndani ya Tanzania. Hivyo kwa awamu ya kwanza, MV Mama event itafanyika katika mkoa wa Dar Es Salaam katikati ya mwezi wa tano 2016.
Hivyo basi Tanzania Marine Swimming Clabu inatoa nafasi kwa wanawake kuanzia miaka 18 na kuendelea kujitokeza kwa ajili ya mafunzo haya.
Mafunzo yatatolewa bure kwa muda wa siku mbili kulingana na ratiba itakavyopangwa hapo baadae.
KWA WANAWAKE AMBAO WAPO TAYARI KUSHIRIKI KATIKA MAFUNZO HAYA, WANAOMBWA KUWASILIANA NASI KUPITIA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO:
0717252522 au 0752338555 au 0713311009 au 0786275152 au 0713610156.
KARIBUNI SANA.
No comments:
Post a Comment