TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - PRESS RELEASE.
Kikao kilichofanyika tarehe 27 mwezi Machi 2013 katika
ukumbi wa Navy Beach Kigamboni juu ya maandalizi ya event ya Mv Mama.
Pili Omari - Mrs Major General SS Omar (Tanzania Navy Commander) ambaye ni
mshauri mkuu wa event ya Mv Mama alisema, ameona umuhimu wa yeye kushiriki na
kuwashauri akinamama waanzishe event ya kuwafundisha akimama wenzao jinsi ya
kuogelea na kujiokoa na majanga ya maji "mara nyingi kati ya ajali mbaya
zinazotokea za mafuriko, kuzama kwa meli nk. waathirika wakubwa ni akinamama na
watoto pia amewashukuru akinamama waliokubali kuunda kamati hiyo na kuwasaidia
wananwake wenzao, na ametoa wito kwa wafadhili mbalimbali, taasisi, makampuni
na watu binafsi kujitolea kuwezesha na kufanikisha event ya Mv Mama.
katika kuhakikisha event hii inafanikiwa vilivyo mama SS Omar
(mshauri mkuu) amewataka akina baba wawaruhusu akinamama hao kushiriki katika
event ya Mv mama bila vipingamizi.
Kwa upande wake Bi. Beatrice Mkunde ( Mhadhiri wa chuo cha
Mwalimu Nyerere) ambaye ni katibu wa kamati hiyo alisema kamati ya akinamama
hao imejipanga kikamilifu kuhakikisha event ya Mv Mama inafanikiwa kwa
mafanikio makubwa. Event ya Mv Mama inatarajiwa kufanyika mwezi wa tano mwaka
2013 huko kigamboni.
Akifafanua zaidi mkufunzi mkuu atakayeendesha event ya Mv Mama Bw. Geofrey
Kimimba Mwakabende toka klabu ya Tanzania Marine Swimming alisema kuwa Mv Mama imetokana
na jina la Meli ambayo inatumia nafsi ya kike kwa maana ya kwamba Meli sawa na
mama kiusafi, uwezo wa ubebaji na utendaji
kazi kwa ujumla. Hivyo MV Mama itakuwa ni ujuzi ambao anaenda kupatiwa mwanamke
kwa event hii ya kwanza lakini kwakutambua kuwa ukimuelimisha mwanamke
umeelimisha jamii au ulimwengu mzima hivyo itaendelea kuwaelimisha hata wanaume
na watu wa rika na jinsia zote kwa event zitakazofuata chini ya MV mama.
Mkufunzi huyo alisema kuwa kwa uzoefu wa klabu yake watu ambao wamekuwa wakijitokeza kwa
wingi kwenye event mbalimbali walizowahi
kuandaa ni wanaume zaidi kutokana na sababu za kihistoria, na kiutamaduni ambapo wanawake wamekuwa wakipewa kazi za
kwenda porini kuokota kuni ilihali wanaume wakifanya kazi za kuogelea na
hatimae kuwa wavuvi na hivyo kupelekea kuwa mwanamke u binti wakitanzania
akionekana kama ni mhuni au mtu anepotoka kimaadili pale anapoonekana akiogelea,
licha ya mabadiliko tulionayo hivi sasa ambapo mwanamke ndiye anayewajibika
mara nyingi na watoto pale anapokuwa anaenda nao beach, kuchota maji mtoni, na kuwavusha mto. Pia wanawake na watoto ndio waathirika
wakubwa wa mafuriko,na ajali za majini
ambazo zimewahi kutokea hapa Tanzania.
Kwa mujibu wa mkufunzi mkuu wa klabu ya Tanzania Marine
Swimming katika event ya MV Mama mambo yatakayofundishwa ni pamoja na;
- Kanuni za usalama majini
- Kuogelea
- Jinsi ya kumuokoa mtu anaekufa maji
- Jinsi ya kutoa msaada kwa aliyeokolewa kwenye maji
- Mbinu za kuvuka mito
- Utumiaji wa vifaa vyakujiokolea
- Jinsi ya kuihama meli
- Jinsi yakusubiri msaada majini
- Jinsi yakutunza mazingira ya maji na yale yanayozunguka vyanzo vya maji
Mwisho kabisa ni wito kwa wafadhili, watanzania, na
watu mbali mbali katika jamii kutambua
umuhimu wa mafunzo haya na kujitoa kwa hali na mali kuweza kufanikisha na kufanya mafunzo kama haya kuwa endelevu na
kuweza kusaidia watanzania wengi zaidi
kunufaika nayo.
Marine Tanzania
Swimming Club
+255 714 287 207
+255 788 343 051
+255 713 311 009
Tarehe 27 Machi 2013
No comments:
Post a Comment