Tuesday 29 March 2016

Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na maeneo mengi ya maji kama vile mito, maziwa, mabwawa na bahari. Maeneo haya ya maji, yamekuwa ni sehemu mojawapo inayotumiwa na watanzania kwa usafiri pamoja na shughuli zingine za kijamii kama vile uvuvi na kadhalika.
Pamoja na utajiri huu ambao tumetunukiwa na Mungu, Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kwa vifo visivyokuwa vya lazima vitokanavyo na ajali za majini na majanga mengine ya maji kama vile mafuriko. Hata hivyo historia inaonesha kuwa katika ajali za majini, watu wengi wanaopoteza maisha huwa ni wanawake na watoto.
Idadi hii inakuwa kubwa kutokana na ukweli usiopingika kuwa, wanawake wengi hawana uelewa wa kitaalamu kuhusu namna ya kujiokoa katika majanga ya maji, hawana uelewa kuhusu namna ya kukaa katika maji kwa muda mrefu ili kusubiri msaada panapotokea matatizo ya majini, vilevile hawana uelewa ni namna gani ya kutoa msaada kwa mtu aliyezama maji. Kutokuelewa kwa mambo haya, kunasababisha mwanamke awe muoga katika kupambana na majanga ya maji, hivyo kuwa ni muhanga mkubwa katika majanga yatokananyo na maji.
Hivyo basi kutokana na tatizo hili lililopo katika jamii yetu ya kitanzania, na kwa kuwa TANZANIA MARINE SWIMMING CLUB inayo wataalamu wenye uelewa wa majanga ya maji na ambao wameshahusika katika shughuli za uokoaji katika mafurika ambayo yalishawahi kutokea maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania, Tanzania Marine Swimming Club imeamua kuanzisha “program” iitwayo MV MAMA.

MV mama ni programu inayohusika na utoaji wa elimu kwa nadharia na vitendo kwa wanawake, kuhusu namna ya kujiokoa na majanga ya maji. 
Programu hii ya MV mama, itakuwa na "Event" ambazo zitafanyika katika nyakati tofauti na mikoa tofauti ndani ya Tanzania. Hivyo kwa awamu ya kwanza, MV Mama event itafanyika katika mkoa wa Dar Es Salaam katikati ya mwezi wa tano 2016.
Hivyo basi Tanzania Marine Swimming Clabu inatoa nafasi kwa wanawake kuanzia miaka 18 na kuendelea kujitokeza kwa ajili ya mafunzo haya.
Mafunzo yatatolewa bure kwa muda wa siku mbili kulingana na ratiba itakavyopangwa hapo baadae.
KWA WANAWAKE AMBAO WAPO TAYARI KUSHIRIKI KATIKA MAFUNZO HAYA, WANAOMBWA KUWASILIANA NASI KUPITIA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO: 
0717252522 au 0752338555 au 0713311009 au 0786275152 au 0713610156.
                                                        KARIBUNI SANA.

Popular Posts